Je ina maana gani kwamba Yesu ni Mwana-kondoo wa Mungu?Yesu anaitwa Mwana-kondoo wa Mungu katika Yohana 1:29 na Yohana 1:36, inamtaja Yeye kama sadaka kamili na ya mwisho kwa ajili ya dhambi. Ili uelewa Kristo alikuwa nani na alifanya nini, ni lazima tuanze na Agano la Kale, ambayo ina unabii kuhusu kuja wa Kristo kama " sadaka ya hatia " ( Isaya 53:10). Kwa kweli, mfumo mzima wa sadaka imara uliowekwa na Mungu katika Agano la Kale unaweka msingi kwa kuja kwa Yesu Kristo, ambaye ni sadaka kamili ya Mungu anaitoa kama upatanisho naye kwa ajili ya dhambi za zetu (Warumi 8:3, Waebrania 10). Sadaka ya kondoo ilikua na jukumu muhimu sana katika maisha ya kidini ya Wayahudi na mfumo wa sadaka. Wakati Yohana Mbatizaji anamrejelea Yesu kama " Mwana-kondoo wa Mungu aondoaye dhambi ya ulimwengu" (Yohana 1:29), Wayahudi waliomsikia wangeweza fikiria kuwa ni mojawapo wa sadaka yoyote muhimu katika sadaka nyingi walizo kuwa nazo. Huku muda wa sikukuu ya Pasaka ukiwa karibu sana, mawazo ya kwanza yanaweza kuwa ni kondoo wa pasaka. Sikukuu ya Pasaka ilikuwa mojapo ya likizo kuu ya Wayahudi na sherehe katika kumkumbuka ya ukombozi wa Mungu kwa Waisraeli kutoka katika utumwani Misri. Kwa kweli, ujijanji wa kondoo ya Pasaka na kupaka damu katika miimo ya nyumba (Kutoka 12:11-13) ni picha nzuri ya kazi ya upatanisho wa Kristo juu ya msalaba. Wale ambao alifia wafunikwa kwa damu yake, ikitulinda sisi kutokana na malaika wa (kiroho) kifo. Sadaka nyingine muhimu inayohusisha kondoo ilikuwa sadaka ya kila siku katika hekalu ya Yerusalemu. Kila asubuhi na jioni, kondoo alitowa sadaka katika hekalu kwa ajili ya dhambi za watu (Kutoka 29:38-42). Hizi dhabihu za kila siku, kama zile zingine zote, zilikuwa tu zinatuelekeza kwa sadaka kamili ya Kristo juu ya msalaba. Kwa kweli, wakati wa kifo cha Yesu msalabani kilikuwa sambamba na wakati wa sadaka ya jioni alipotolewa katika hekalu. Wayahudi wa wakati huo pia walimjua nabii Yeremia na Isaya wa Agano la Kale la, waliotangaza mbeleni ya kuja kwa Yule atakayeletwa " kama mwana-kondoo anayepelekwa kuchinjwa" (Yeremia 11:19; Isaya 53:7 ) na ambaye mateso na sadaka yake itatoa ukombozi kwa ajili ya Israeli. Bila shaka, mtu huyo hakuwa mwingine ila tu ni Yesu Kristo, " Mwana-kondoo wa Mungu." Wakati wazo la mfumo wa kafara linaweza kuonekana la ajabu kwetu hii leo, dhana ya malipo au ukombozi bado ni moja tunaweza kuielewa kwa urahisi. Tunajua kwamba mshahara wa dhambi ni mauti (Warumi 6:23) na dhambi zetu zinatutenga kutoka kwa Mungu. Tunajua pia Biblia inafundisha kuwa sisi ni wenye dhambi na hakuna hata mmoja wetu ni wa haki mbele za Mungu (Warumi 3:23). Kwa sababu ya dhambi zetu, sisi tumetengwa kutoka kwa Mungu, na kusimama na hatia mbele zake. Kwa hiyo, tumaini tunaloweza kuwa nalo ni kama Yeye atatoa njia ambayo sisi tutapatanishwa naye, na hicho ndicho alichokitenda kwa kumtuma Mwanawe Yesu Kristo kufa juu ya msalaba. Kristo alikufa ili afanye upatanisho kwa ajili ya dhambi zetu na kulipa adhabu ya dhambi za wote ambao wanamwamini. Ni kupitia kwa kifo chake msalabani kama dhabihu kamilifu ya Mungu kwa ajili ya dhambi na kufufuka kwake siku tatu baadaye kwamba sasa tunaweza kuwa na uzima wa milele kama tutamwamini Yeye. Ukweli kwamba Mungu mwenyewe ametoa sadaka ambayo inaosha dhambi zetu ni sehemu ya utukufu ya habari njema ya injili ambayo imewekwa wazi kabisa katika 1 Petro 1:18-21: "Nanyi mfahamu kwamba mlikombolewa si kwa vitu viharibikavyo, kwa fedha au dhahabu, mpate kutoka katika mwenendo wenu usiofaa mlioupokea kwa baba zenu; bali kwa damu ya thamani, kama ya mwana-kondoo asiye na ila, asiye na waa, yaani, ya Kristo. Naye amejulikana kweli tangu zamani, kabla haijawekwa misingi ya dunia; lakini alifunuliwa mwisho wa zamani kwa ajili yenu; ambao kwa yeye mmekuwa wenye kumwamini Mungu, aliyemfufua katika wafu akampa utukufu; hata imani yeunu na tumaini lenu liwe kwa Mungu." |